Wananchi wameanza vyema raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Merrikh katika mchezo uliopigwa uwanja wa Pele, Rwanda
Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Jannedy Musonda na Clement Mzize yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu wa ugenini ambao unawaweka katiika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi
Pengine ni mchezo ambao Yanga ilistahili kuibuka na ushindi mnono zaidi kwani Wananchi walitawala na kutengeneza nafasi nyingi
Mzize alipoteza nafasi adimu kama ilivyo kwa Aziz Ki ambaye hata hivyo alitoa pasi ya bao la pili kwa kisigino, Mzize aliweka mpira kimiani
Yanga inahitaji kumaliza kazi katika mchezo wa pili ikihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare
Uwanja wa Pele leo ulipendeza kwa rangi za njano na kijani mashabiki wa Yanga wakihanikiza kwa shangwe
Tukutane Dar tumalize kazi...!