Wakati kikosi cha wachezaji kikitua Rwanda jana usiku kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh utakaopigwa uwanja wa Pele hapo kesho, msafara wa mashabiki unatarajiwa kuingia Rwanda leo
Pengine inaweza kuwa rekodi Afrika kwa idadi kubwa ya mashabiki kusafiri kwa mabasi kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa ajili ya kuishangilia timu yao
Zaidi ya mabasi 50 yataingia Rwanda leo yakiwa na mashabiki wa Yanga ambao kesho watakuwa na kazi ya kuiongezea hamasa timu yao ili kuhakikisha inashinda
Aidha shamra shamra kuelekea mchezo huo pia zimewashtua Wanyarwanda wenyewe kwani hawakuwahi kushuhudia 'vibe' la mashabiki wa soka kama hili wanaloliona kutoka kwa Wananchi
Licha ya Al Merrikh kuweka viingilio vikubwa katika mchezo huo ambapo kiingilio cha chini ni Tsh 21,000/-, watarajie uwanja wa Pele unaochukua mashabiki 22,000 kujaa
Hii ndio Yanga, klabu namba 3 kwa ubora barani Afrika...!