Walinzi wa Yanga Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job jana walikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kilichofuzu michuano ya Afcon 2023 baada ya suluhu ya bila ya kufungana dhidi ya miamba wa soka Algeria
Kazi kubwa ilifanywa na wachezaji wote wa Stars lakini utakuwa mchoyo wa fadhila kama hutawapa kongole Mwamnyeto, Bacca na Job kwa kazi nzuri waliofanya kwenye safu ya ulinzi
Sio bahati mbaya kwa kocha wa Stars Adel Amrauche kuwaamini nyota hao kwani anaifahamu kazi yao katika kikosi cha Yanga
Ukuta wa Yanga haujaruhusu bao lolote kwenye ligi msimu huu, wakiruhusu bao moja tu katika mechi sita zilizopita
ADVERTISE HERE