Kwa mara nyingine uongozi wa Yanga umefanya jitihada kukisuka upya kikosi cha Yanga Princess ili kuhakikisha wanafanya vizuri ligi kuu ya Wanawake msimu ujao
Msimu uliopita Yanga Princess ilisajili nyota wengi wa kigeni hata hivyo hawakuweza kuisaidia Yanga Princess kufikia malengo yake
Wakati huu imefanyika 'scouting' kubwa, matumaini ni kuwa wachezaji waliosajiliwa chini ya Kocha Mkuu Charles Haalubono kutoka Zambia, wataenda kuwapa furaha Wananchi
Yanga Princess ilitangaza kuachana na wachezaji 13, wengi wao wakiwa wa kigeni na juzi ilianza kutambulisha wachezaji waliosajiliwa kuchukua nafasi zao
Adejoke Ejalonibu, kiungo mshambuliaji raia wa Nigeria kutoka Raja Casablanca alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa
Jana Yanga Princess ikatambulisha nyota wengine wawili wa kigeni mshambuliaji Faiza Seidu raia wa Ghana ambaye pia hucheza timu ya Taifa ya Ghana

Katika msimu uliopita, Faiza alishika nafasi ya tatu ya ufungaji bora katika ligi ya wanawake nchini Ghana akimaliza ligi na magoli 15
Yanga Princess pia ilitambulisha usajili wa kiungo fundi Madina Traore raia wa Burkina Faso

Wachezaji wote waliosajiliwa mpaka sasa wanazitumikia timu zao za Taifa
Majira ya saa 1 usiku Yanga Princess ikatambulisha usajili wa mshambuliaji Neema Paul aliyetua kutoka Fountain Gate Princess