Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameendeleza utaratibu wa 'rotation' ya kikosi chake ambapo mpaka sasa msimu huu katika mashindano yote, ametumia wachezaji 26 kati ya 28 waliosajiliwa
Kuanzia Ngao ya Jamii, ni wachezaji wawili tu ambao bado hawajapata nafasi ya kucheza ambao ni mlinda lango Aboutwalib Mshery aliyerejea kikosini bada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi sita na beki wa kati Shaibu aliyepandishwa kutoka timu ya vijana U20
Skudu Makudubela alitumika kwa dakika 7 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc akapata majeraha ambayo yalimfanya akose mechi zilizofuata. Lakini tayari amepona na anatarajiwa kuanza mazoezi ya timu
Pamoja na kufanya 'rotation' ya kikosi chake kutoka mchezo mmoja kwenda mwingine, kasi ya Yanga haijabadilika
Licha ya kucheza mechi nne katika muda wa siku tisa, Yanga imeshinda mechi zote huku ikifunga mabao 17 na kuruhusu bao moja tu
Kama sio upana wa kikosi, pengine isingekuwa rahisi kama inavyoonekana, Wananchi wakifunga mabao matano katika kila mechi kwenye mechi tatu za mwisho
Aidha katika magoli 17 yaliyofungwa, magoli mawili yamefungwa na mabeki, magoli matano yamefungwa na Washambuliaji na magoli kumi yaliobaki yamefungwa na viungo
Jumla ya wachezaji 9 wamehusika kwenye kufunga magoli 17 katika mechi nne zilizopita
Hii ndio tafsiri sahihi ya kikosi kipana, hakuna utegemezi wa mchezaji mmoja