Maxi tuzo ya ligi kuu August inamuhusu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2023
Maxi tuzo ya ligi kuu August inamuhusu

Kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli jana aliendeleza moto wake katika kikosi cha Yanga akiwasaidia Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Katika dakika 90 za mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Maxi alipachika mabao mawili huku pia akitoa pasi moja ya bao

Kwenye mechi mbili za Ligi Kuu, Maxi amehusika katika mabao manne kwani pia alitoa assist katika mchezo dhidi ya KMC

Katika mechi tatu, Maxi amehusika katika mabao saba kwani kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc, pia alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao

Maxi na Yao Yao jana waling'ara katika mchezo ambao licha ya jitihada ambazo JKT Tanzania walifanya kwenye kipindi cha kwanza kujinusuru na kipigo, haikuwezekana!

Mazxi ni mchezaji wa aina yake katika kikosi cha Yanga, sio rahisi kufahamu anacheza namba ngapi uwanjani kwani yuko kila mahali...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’