Kiungo Thabani Kamusoko alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotoka suluhu ya bila kufungana na Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa nchini Botswana Jumamosi iliyopita.
Kamusoko ambaye amerejea dimbani hivi karibuni baada ya kuwa majeruhi kwa miezi minne alicheza kwa dakika 65 kabla hajampisha Ibrahim Ajib.
Kiungo huyo fundi ameanza kurejea katika kiwango chake na mwenyewe amefurahia hali hiyo.
"Polepole naanza kurejea, ninaridhishwa na maendeleo yangu," ameandika Kamusoko kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Wakati Kamusoko akirejea na kuanza kuitumikia Yanga kikamilifu, Amissi Tambwe na Donald Ngoma nao wanatarajiwa kuwa kikosini mapema mwezi ujao.
Kwa sasa michuano yote imesimama kwa wiki mbili kupisha michezo ya kimataifa ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA

ADVERTISE HERE