Tumepata somo ligi ya mabingwa - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
20 Mar 2018
Tumepata somo ligi ya mabingwa - Lwandamina
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema kwamba watajitahidi wasirudie makosa ili wakate ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tunahamia kwenye Kombe la Shirikisho, huko tunakwenda kwa nguvu zote na kiu ya kufanya vizuri baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa,”amesema Lwandamina.

Mzambia huyo amesema anaamini vijana wake wamepata somo baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa watakuwa makini wasirudie makosa.

Yanga SC imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.

Yanga SC wameangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Pamoja na Kombe la Shirikisho, Yanga pia wapo kwenye mbio za mataji mengine mawili nyumbani, Ligi Kuu na Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Katika Ligi wapo nyuma ya Simba SC wanaoongoza pointi 46 baada ya kucheza mechi 20, wakati mabingwa hao watetezi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 46 pia baada ya kucheza mechi 21, wakiwa wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kwenye Azam Sports Federation Cup Yanga wapo Robo Fainali ambako watamenyana na Singida United Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Namfua mjini Singida.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →