Asanteni Wananchi kwa heshima kubwa - Maxi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2023
Asanteni Wananchi kwa heshima kubwa - Maxi

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Mpia Nzengeli amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti kubwa waliowapa wachezaji katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Asas Fc

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1

Mchezo huo ulikuwa maalum kwa Maxi, mashabiki wakichomokea mavazi yao ikiwa ishara ya kumuunga mkono

"Nawashukuru mashabiki wa Yanga kwa tukio hili walilofanya nafikiri litabaki katika kumbukumbu ya maisha yangu kwa muda mrefu. Nimeona hamasa kubwa kabla ya mchezo na kuendelea siku ya mchezo"

"Katika maisha yangu hii ni mara ya kwanza kukutana na tukio kama hili, hii ni heshima kubwa kwangu"

"Ninachowaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono wachezaji wote na matukio haya yaendelee kwa kila mchezaji," alisema Maxi

Naye Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema matukio maalum ya kuwaongezea thamani wachezaji yataendelea kwenye mechi zote za Kimataifa

"Huu ni mwanzo tu, tutaendelea kwa wachezaji wengine wote. Kutakuwa na siku ya Zouzoua na hapa nimepokea meseji nyingi kutoka kwa kinadada wanataka itakayofuata iwe maalum kwa Aziz Ki sijajua wanataka kufanya nini siku hiyo," alibainisha Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’