El Merreikh imetangulia raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikibebwa na faida ya bao la ugenini dhidi ya Otoho
Mchezo uliopigwa leo uwanja wa Huye huko Rwanda El Merreikh wakiwa wenyeji ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Mchezo wa kwanza uliopigwa Congo Brazaville Otoho wakiwa wenyeji ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
El Merreikh watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Asas Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex
Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Rwanda na marudiano kupigwa jijini Dar es salaam uwanja wa Azam Complex
ADVERTISE HERE