Yanga kujipanga itinge makundi Shirikisho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2018
Yanga kujipanga itinge makundi Shirikisho
Siku chache baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kukutana na benchi la ufundi ili kuangalia sababu zinazopelekea kutofanya vizuri kwenye michezo ya nyumbani kwenye ushiriki wao wa michuano ya kimataifa.

Yanga Jumamosi iliyopita iliwabana wenyeji wao Township Rollers na kulazimisha suluhu, lakini ilikubali kipigo cha mabao 2-1 nyumbani kwenye michuano hiyo.

Kuondolewa huko kunaifanya Yanga sasa kutupwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano Hussein Nyika, alisema kuwa kamati hiyo leo itakutana na benchi la ufundi kufanya tathimini ya ushiriki wao.

"Bado tupo kwenye michuano ya kimataifa, lakini ni lazima tuangalie ni kwa nini tunakwama nyumbani kupata ushindi, tulicheza vizuri sana Botswana, vile tulivyocheza kule kama tungefanya hivyo hapa nyumbani tungesonga mbele," alisema Nyika.

"Tutakutana na benchi la ufundi, na tutaweka mikakati ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye kombe la Shirikisho," alisema Nyika.

Aidha, alisema malengo yao kwenye michuano hiyo ni kufika hatua ya makundi.

"Kwanza lazima tufike hatua ya makundi, hayo ndio malengo, tunajipanga na baada ya kukutana na benchi la ufundi tutajua nini cha kufanya," alisema Nyika.

Nyika, alisema kwenye kikao hicho pia watapokea maoni ya kocha wao juu ya maandalizi ya ushiriki wa kombe la Shirikisho kama ataamua timu ikakae kambini au vinginevyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’