Maxi kuendeleza kasi ya kupika mabao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2023
Maxi kuendeleza kasi ya kupika mabao

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Maxi Nzengeli amesema kuwa anataka kuendeleza moto wa rekodi yake ya kuwa kinara wa kutoa pasi za mabao aliyoiacha nchini kwao, DR Congo alipokuwa akiichezea Maniema FC

Maxi anasema ingawa mashabiki wa Yanga wamempokea vizuri tangu alipoanza kucheza, lakini bado hajaanza kwa kasi ya kuzalisha mabao, ingawa ameshafanya hivyo mara mbili tatu

Akicheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Maxi alitoa pasi yake ya kwanza ya bao pekee la ushindi, lakini pia akatoa pasi yake ya pili dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, iliyotumiwa na Stephanie Azizi KI

Katika mchezo dhidi ya KMC, Max alitoa pasi ya goli la tano lililofungwa na Pacome Zouzoua. Kiungo huyo amesema tayari wameanza kuzoeana ndani ya kikosi chao na kuanza kwa ligi anataka kufufua ubora wake huo ambao utaisaidia timu

"Naweza kutoa pasi za mabao na hata kufunga, unajua hapa Yanga ndiyo nilikuwa nafika, ilihitaji muda kidogo kuzoeana na wenzangu vile wanavyocheza, kitu ambacho sasa kimeanza kukaa sawa"

"Tuna timu nzuri ambayo kila mchezaji ana ubora mkubwa, naamini mabao yataanza kuja kwa wingi muda si mrefu, kwangu kitu nataka kukifanya ni kuendeleza rekodi yangu ya kuzalisha pasi za mabao na hata kufunga ili kusaidia timu," alisema Maxi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
35m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’