Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Scudu Makudubela anatarajiwa kurudi nchini kesho Ijumaa akitokea kwao Afrika Kusini alipokwenda kubadili hati yake ya Kusafiria (Passport)
Nyota huyo aliondoka nchini wiki iliyopita akipea ruhusa na uongozi ili kushughulikia hati yake ya kusafiria iliyokuwa imejaa
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema Skudu atatua nchini kesho
"Nitawaambia ndugu zangu Waandishi muda ambao Scudu anarudi kesho na muende, sio mnamrekodi picha za kiujanja ujanja, huyu alikwenda kwao kubadili Passport yake" alisema Kamwe
ADVERTISE HERE