Mshambuliaji mpya wa Yanga Hafiz Konkoni jana alifungua akaunti yake ya mabao katika ligi kuu ya NBC akifunga bao la tatu katika ushindi wa mabao 5-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya KMC
Konkoni aliyeingia dakika ya 64 kuchukua nafasi ya Kennedy Musonda, alifunga bao hilo baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa KMC kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Aziz Ki
Konkoni pia alitoa pasi ya bao la nne lililofungwa na Mudathir Yahya baada ya Yanga kufanya 'pressing' kwenye lango la KMC na kuwapora mpira
Konkoni amesema bao hilo ni muhimu sana kwake kwani limempunguzia presha hasa kwa kufahamu usajili wake ni maalum kuchukua nafasi ya Fiston Mayele aliyefanya mambo makubwa akiwa Yanga
"Kusajiliwa na Yanga kuchukua nafasi ya mmoja wa washambuliaji bora barani Afrika Fiston Mayele huku ukifahamu mashabiki watataka ufanya kama yeye au zaidi, ni jambo linalokuja na presha kubwa"
"Nilihitaji kufunga bao ili kuondoa hiyo presha nashukuru nimefanikiwa, umekuwa mwanzo mzuri kwangu," alisema Konkoni