Mashabiki wa Yanga wanashauku ya kumuona uwanjani kwa muda mrefu zaidi mshambuliaji Hafiz Konkoni
Konkoni alipewa takribani dakika 15 katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc, wengi walifurahishwa na kile alichoonyesha
Pengine leo Kocha Miguel Gamondi anaweza kumpa dakika nyingi zaidi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex
Gamondi aliweka msimamo kwa wachezaji waliochelewa kujiunga na wenzao katika pre-season kuwa lazima wapate muda wa kufanya mazoezi zaidi kabla ya kuanza kutumika

Ilikuwa hivyo kwa kiungo fundi Pacome Zouzoua ambaye alipewa dakika chache katika Ngao ya Jamii na kupewa muda mrefu zaidi katika mchezo dhidi ya Asas
Wachezaji hao wote sasa wako tayari pengine Wananchi watarajie kuwashuhudia dimba la Azam Complex baadae leo