Hakuna taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga juu ya kumuhitaji mshambuliaji Saimon Msuva
Mara kadhaa Msuva ameweka wazi msimamo wake kuwa bado malengo yake ni kucheza nje ya Tanzania
Bado msimamo wake ni huo hivyo ni wazi taarifa zinazomuhusisha na klabu ya Yanga ni tetesi tu
Lakini bado dirisha la usajili kwa wachezaji wa ndani halijafungwa, Yanga inayo nafasi ya kujiimarisha kama Kocha Miguel Gamondi atahitaji
Kwa michuano ya CAF, dirisha lilifungwa Julai 31 lakini nafasi ya kusajili bado ipo ambapo timu inayohitaji kuongeza mchezaji (kama haijatimiza idadi wachezaji 40) inaweza kusajili kwa kulipia gharama lakini mchezaji huyo anaweza kutumika kuanzia hatua ya makundi
ADVERTISE HERE