Yao Kouassi 'Yao-Yao' ameshindikana! Kwa mlinzi huyu wa kulia Yanga imesajili mchezaji kwelikweli
Haijawahi kuwa rahisi kwa wachezaji wa timu pinzani ambao wanacheza upande wa kulia
Sio winga au mlinzi wa pembeni! Yao akiifungulia 'turbo' yake hazuiliki
Wakati mwingine unaweza usielewe anacheza namba ngapi? utamuona kwenye ulinzi timu ikiwa inashambuliwa na pia utamuona eneo la wapinzani timu ikiwa inashambulia
Yao atakuwa mwalimu mzuri wa Kibwana Shomari na walinzi wengine wa pembeni vile wanapaswa kucheza katika nafasi hiyo
Kwa 'shughuli' zake hakuna winga wala beki wa timu pinzani ambaye atatamani kucheza upande wake
Wananchi wanamuita 'JESHI', mwamba asiyetaka masihara kazini...!
ADVERTISE HERE