Winga wa Yanga Skudu Makudubela amerejea Afrika Kusini kwa ajili ya kuhuisha hati yake ya kusafiria
Skudu aliondoka nchini Alfajiri ya jana kuwahi kuhuisha hati yake ya kusafiria ambayo imejaa
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali kamwe amesema benchi la ufundi limeona ni wakati sahihi kwa nyota huyo kwenda kuhuisha hati yake ya kusafiria kabla ratiba ya michuano ya Kimataifa haijachanganya
Skudu alirejea kikosini hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya goti aliyopata katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc wiki iliyopita
Anatarajiwa kurejea nchini August 24 kuwahi mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc
ADVERTISE HERE