Kile alichoonyesha Stephane Aziz Ki kwenye mechi mbili za Ngao ya Jamii, kimewapa imani Wananchi kuwa msimu huu unaweza kuwa bora zaidi kwa fundi huyo anayetumia mguu wa kushoto wenye maajabu
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alimtumia Aziz Ki kwa takribani dakika 60 tu kwa mechi zote mbili za Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc na Simba
Gamondi alieleza sababu kwa nini Aziz Ki na baadhi ya wachezaji kama Pacome Zouzoua na Hafiz Konkoni hawakupata muda mrefu kwenye michuano hiyo kwa sababu hawana 'fitness' ya kutosha kwa kuwa walichelewa kujiunga na wenzao kwenye pre-season
Aziz Ki na Maxi Nzengeli wanaweza kuwa wachezaji muhimu sana wa Yanga katika msimu huu kwenye upishi wa mabao
Wawili hao walikuwa na mchango mkubwa katika mchezo dhidi ya Azam Fc na hata alipoingia Aziz Ki katika mchezo dhidi ya Simba, nafasi nyingi zaidi zlitengenezwa kupitia ushirikiano wao
Wananchi wanasubiri kwa hamu siku ambayo Gamondi ataamua kuwatumia Aziz Ki, Pacome na Maxi kwa muda mrefu zaidi uwanjani kama alivyofanya dakika za mwisho katika mchezo dhidi ya Simba
Kwa sababu ni wachezaji wenye ufundi mkubwa mguuni ambao wanaweza kurahisisha kufungua safu za timu pinzani na kutengeneza mabao