Nani anaanza, nani anasubiri vs Simba leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Aug 2023
Nani anaanza, nani anasubiri vs Simba leo?

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo ana kazi ya kuamua wachezaji 11 ambao wataanza katika mchezo wa fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani

Gamondi anakabiliwa na mtihani huo kutokana na ubora wa kikosi chake. Katika kila nafasi Yanga ina wachezaji wawili ambao wanakaribiana ubora

Katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc, Gamondi alianza na wachezaji wapya watatu Skudu, Maxi Nzengeli na Yao

Baadae Skudu alitoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Crispine Ngushi

Leo huenda Wananchi wakashuhudia mabadiliko katika baadhi ya nafasi ili kuongeza ubora zaidi katika mchezo huo wa fainali

Nyota wapya beki Gift Fred, mshambuliaji Hafiz Konkoni na kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua wanaweza kujumuishwa katika kikosi cha leo

Wachezaji hao hawakuwa sehemu ya kikosi kilichoikabili Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Clement Mzize alikuwa na kiwango bora katika mchezo uliopita, haitashangaza leo kama Gamondi ataamua kumuanzisha na pengine Kennedy Musonda akaanzia winga ya kushoto nafasi ya Skudu ambaye majeraha aliyopata mchezo uliopita yanaweza kumuweka nje licha ya kuanza mazoezi mepesi

Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kutetea Ngao ya Jamii kwa msimu wa tatu, matokeo ambayo yatadhihirisha umwamba wao mbele ya watani zao Simba

Yanga wametwaa Ngao mbili katika misimu miwili iliyopita kwa ushindi dhidi ya Simba, wakishinda leo utakuwa ushindi wa tatu mfululizo mbele ya watani zao hao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’