Licha ya kukaa nje kwa mwezi mzima kutokana na majeruhi, beki Andrew Vicent Chikupe jana aliibuka nyota wa mchezo kwa upande wa kikosi cha Yanga kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Uwepo wa Chikupe kwenye mchezo huo uliongeza umakini katika safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa imara sana.
Said Juma Makapu amekuwa akitumika kwenye nafasi ya ulinzi wakati wote ambao Dante amekosekana kikosini.
Kurejea kwake kulimpa nafasi Makapu kucheza namba ya kiungo mkabaji ambayo ndio anayoimudu zaidi
Ni dhahiri kukosekana kwa Chikupe katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam kulichangia kwa kiasi kikubwa Yanga kuruhusu mabao mawili yaliyoigharimu nafasi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kabla ya kuumia mwezi uliopita, Chikupe alikuwa mchezaji pekee wa Yanga aliyekuwa amecheza michezo mingi zaidi msimu huu.
Kurejea kwake kikosini ni habari njema kwa Yanga ambayo inakabiliwa na michuano mitatu ya ligi, kombe la FA na raundi ya mtoano kombe la Shirikisho.

ADVERTISE HERE