Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya wachezaji wao wa kigeni baada ya mapema leo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoa taarifa kuwa halitaruhusu wachezaji wa kigeni ambao hawana vibali kushiriki Ngao ya Jamii
Katika taarifa hiyo, klabu za Yanga, Simba na Singida FG zilitajwa kutowasilisha vibali vya wachezaji wao TFF hivyo hazipaswi kuwatumia
"Na tutawaanzisha wote," aliandika Kamwe kwa ufupi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wakati akijibu andiko la TFF
Imeelezwa tayari Yanga imewasilisha vibali vya wachezaji wake wote 12 wa kigeni hivyo wanaweza kutumika kwenye Ngao ya Jamii
Majira ya saa 1 usiku Yanga itashuka uwanja wa Mkwakwani kupepetana na Azam Fc katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali
