Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa klabu ambayo haikuwasilisha vibali vya wachezaji wake wa kigeni, haitaruhusiwa kuwatumia katika mechi za Ngao ya Jamii zinazoanza leo jijini Tanga
Yanga itashuka dimbani majira ya saa 1 usiku kuikabili Azam FC katika mchezo wa nusu fainali
Taarifa iliyotolewa na TFF, imebainisha kuwa ni Azam Fc pekee iliyowasilisha vibali vya wachezaji wake 10 wa kigeni
Klabu za Yanga, Simba na Singida FG hazijawasilisha. Bila shaka uongozi wa Yanga utamaliza hili mapema ili kuweza kuwatumia wachezaji wake wa kigeni katika mchezo dhidi ya Azam FC

ADVERTISE HERE