Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga bado ina kete moja ya kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho CAF CC.
Yanga itacheza mchezo wa mtoano dhidi ya moja ya timu zitakazokuwa zimefuzu raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Droo ya hatua hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Misri katika jiji la Cairo, March 21.
Raundi ya kwanza ya mtoano kombe la Shirikisho itapigwa kati ya April 06-08 wakati michezo ya marudiano itapigwa kati ya April 16-18.
Yanga itaanzia nyumbani.
Timu ambazo tayari zimefuzu raundi ya kwanza kombe la Shirikisho na huenda zikakumbana na Yanga ni pamoja na Al Masry iliyoiondosha Simba kwenye michuano hiyo.
Nyingine ni CR Belouizdad, CS La Mancha, Djoliba, Raja Casablanca, RS Berkane, SuperSport United na Al-Hilal Al-Ubayyid.
Michezo mingine ya kukamilisha raundi ya kwanza inatarajiwa kupigwa leo Jumapili.

ADVERTISE HERE