Tukio rasmi la uzinduzi wa Documentary ya Yanga itafanyika kesho Jumatatu katika Ukumbi wa Sinema Century Cinemax jijini Dar es salaam
Viongozi, Wanachama, Wadau wa Yanga, wasanii mbalimbali wamealikwa kushuhudia uzinduzi huo
Baada ya uzinduzi, Yanga kwa kushirikiana na Azam Media, wamefanikisha Documentary hiyo kupatikana ndani ya Azam Max App ambao unaweza kuiangalia kwa kulipia Tsh 2,500/- tu
Ndani ya Documentary kutakuwa na taarifa za kina kuhusu yaliyojiri msimu wa 2022/23 Yanga ikifanikishwa kushinda mataji yote ya ndani na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza
Mashabiki huona zao la mwisho pale timu inapokuwa uwanjani lakini hawajui nini hufanyika nyuma ya camera katika kuhakikisha timu inapata mafanikio
Documentary ya Yanga inatoa fursa kwa Wananchi kuona yale mapambano yanayofanyika nyuma ya camera hatua kwa hatua mpaka kuishuhudia timu yao ikicheza fainali ya kombe la Shirikisho