Pamoja na kufunga mabao tisa katika ligi kuu ya NBC msimu uliopita, Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki hakufikia hata nusu ya uwezo wake
Aziz Ki amerejea akiwa na ari kubwa kuelekea msimu ujao pengine Wananchi watarajie mambo makubwa zaidi kutoka kwake
Hata hivyo atahitaji kupambana zaidi ili kujihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza kwani ushindani katika eneo analocheza ni mkubwa
Usajili wa wachezaji Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli umeongeza ushindani katika eneo la namba 10

Zouzoua aliyekuwa MVP wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliopita, alicheza pamoja na Aziz Ki katika klabu ya Asec Mimosas
Wawili hao walikuwa na ushindani wakati wako Asec na sasa wamekutana tena Yanga
Baada ya kuonyesha umahiri kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, Max amebadilishiwa majukumu

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anamtumia Maxi kama kiungo mshambuliaji badala ya winga nafasi ambayo alikuwa akicheza wakati yuko Meneama
Maxi ataiongezea Yanga machaguo kwenye eneo la ushambuliaji kwani anamudu kucheza nafasi zote eneo la mbele