Fiston Mayele ameondoka Tanzania lakini amewaachia Wananchi rekodi ya aina yake ambayo watajivunia kwa muda mrefu
Mayele amepachika jumla ya mabao 33 ya ligi kuu katika misimu yake miwili na Yanga huku akitoa pasi 9 za mabao. Katika mashindano yote Mayele alipachika mabao 52
Mataji sita na fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika ni zawadi kubwa kwa Wananchi

Mshambuliaji aliyetua kuchukua nafasi yake Hafiz Konkoni ana kazi ya kuendeleza pale ambapo Mayele ameishia
Hata hivyo Wananchi hawapaswi kumuweka katika presha kubwa Konkoni ili aweze kutimiza majukumu yake vyema
ADVERTISE HERE