Ukizungumzia kikosi kipana basi nenda kwa Wananchi, Yanga Afrika utakiona
Ndio! tangu msimu uliopita Yanga ilijipambanua kwa kuwa na kikosi kipana kilichompa urahisi aliyekuwa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi
Nabi alitengeneza mfumo mzuri wa kuimarisha wachezaji wa ndani, mfumo ambao umeifanya Yanga kuwa kikosi chenye nyota bora zaidi wa ndani
Ni hivi; Yanga inaweza kutumia kikosi chake cha wachezaji wa ndani tu na kuweza kutetea ubingwa wake
Katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alianza na kikosi kilichokuwa wachezaji nane wa ndani
Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Mudathir Yahya, Jonas Mkude na Denis Nkane
Katika kipindi cha pili pia akawapa nafasi Ibrahim Bacca, Salum Abubakar, Farid Mussa, Zawadi Mauya, Clement Mzize na Crispine Ngushi
Hii ni timu ambayo inaweza kuchuana na yeyote katika ligi kuu ya NBC