Haikuwa rahisi kwa Yanga kumsajili mshambuliaji Hafiz Konkoni (23) ambaye msimu uliopita aliuwasha moto kwelikweli kwenye ligi kuu ya Ghana akifunga mabao 15 na kutoa apasi tatu za mabao akizidiwa mabao matatu na mfungaji bora aliyeweka kambani mabao 18
Katika mashindano yote Konkoni alifunga mabao 26 na kutoa pasi 7 za mabao
Kwa mujibu taarifa kutoka Ghana, Mshambuliaji huyo alikuwa akiwania na timu kama Al Hilal (Sudan), ASEC Mimosas (Ivory Coast), Hearts of Oak (Ghana), Future (Misri) na Al Ahli Tripoi ya Libya
Mwezi June 2023, Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Chris Hughton alimjumuisha Konkoni kwenye timu ya taifa, Ghana dhidi ya Madagascar kuwania kufuzu AFCON 2023
Ghana ni miongoni mwa Mataifa yenye wachezaji wengi wanaosakata kabumbu barani Ulaya, kwa mchezaji wa ndani kuitwa timu ya Taifa ya Ghana inakuonyesha sio mchezaji wa kawaida
Ulikuwa uamuzi sahihi kwake kutua Yanga lakini pia kwa Yanga imemuongeza mshambuliaji mwenye 'profile' kubwa katika kikosi chake kuendeleza pale alipoishia Fiston Mayele
