Yanga inafanya kilicho bora, haishindani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jul 2023
Yanga inafanya kilicho bora, haishindani

Kulingana na takwimu za N-Card takribani mashabiki 40,000 walikata tiketi kushuhudia mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi iliyopita

Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Kennedy Musonda akifunga bao hilo akipokea pasi murua kutoka kwa Maxi Nzengeli

Katika Tamasha hilo Yanga iliingiza zaidi ya Tsh Milioni 400 kutokana na mahudhurio yaliyotangazwa, kiingilio cha chini ilikuwa Tsh 10,000/-

Sio sahihi kufananisha Tamasha la Yanga dhidi ya Tamasha ambalo watani zao Simba wametangaza kulifanya mwezi ujao

Tamasha la Yanga lilifana kwa maana mahudhurio yaliridhisha na hata fedha walipata

Simba wamelenga kutaka kuonyesha wao wamefanya kitu kikubwa zaidi kwa kupunguza bei ya viingilio ili wajaze uwanja lakini hawatapata fedha nyingi kama ilivyokuwa kwa Yanga

Lakini pia Yanga waliwakaribisha mabingwa wa kihistoria ligi kuu ya Afrika Kusini Kaizer Chiefs wakati watani zao Simba wamewaalika Power Dynamos kutoka Zambia

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said mara kadhaa ameweka wazi kuhusu msimamo wa uongozi wake ni kufanya kitu bora chenye manufaa kwa klabu na sio kushindana na timu nyingine

Ndio maana wakati huu utaona ni timu nyingine zinazojaribu kushindana na Yanga kwa kufanya kila ambacho Yanga wanafanya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’