Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda amesema anafahamu ukubwa wa majukumu yake katika kikosi cha mabingwa hao wa nchi kuelekea msimu ujao wa mashindano (2023/24)
Baada ya Fiston Mayele kuondoka, Musonda ndiye mshambuliaji anayetizamwa zaidi kufanya majukumu yaliyoachwa na Mcongomani aliyetimikia Pyramids Fc
Musonda alifunga bao pekee la Yanga katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs mwishoni mwa wiki Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0
"Nafahamu nina mtihani mkubwa, juzi nilikuwa nafahamu natazamwa zaidi na hili limekaa kichwani na nitapambana kuwapa raha mashabiki wa Yanga"
"Eneo la ushambuliaji ndio siri kubwa ya ushindi nimefurahi nimepata nafasi ya kufunga japo sio mabao mengi lakini hilo moja limenipa nguvu na imani kuwa inawezekana na nitatakiwa kuwa imara zaidi kwasasabu natazamwa na wengi," alisema Musonda
Yanga inatarajiwa kusajili mshambuliaji mwingine ambaye atashirikiana na Musonda, Clement Mzize na Crispine Ngushi kuongoza safu ya ushambuliaji