Msimu huu Yanga ina walinda lango watatu ambao hakuna shabiki atahoji pale yeyote anapopewa jukumu la kukaa langoni
Bado Djigui Diarra ataendelea kuwa mlinda lango namba moja lakini bila shaka Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery nao watakuwa na nafasi zao
Juzi katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs, Wananchi walimshuhudia Metacha akiwa katika kiwango bora langoni
Diarra ambaye alichelewa kujiunga na wenzake katika pre-season alipata nafasi ya kucheza dakika 10 za mwisho
Mshery amerejea baada ya kukosekana nusu ya msimu uliopita akiwa majeruhi, anaendelea kuimarika
Kwa magolikipa hawa, unaweza kusema Yanga iko katika mikono salama
ADVERTISE HERE