Msimu uliopita utaendelea kubaki kuwa msimu bora katika historia ya Yanga mpaka rekodi hiyo itakapovunja
Pamoja na kushinda mataji yote ya ndani, ni msimu ambao Yanga ilipata mafanikio makubwa zaidi katika michuano klabu barani Afrika kwa kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Almanusra Yanga watwae taji la Shirikisho kama sio sheria ya bao la ugenini ambayo CAF wameendelea kuikumbatia licha ya wanachama wengine wa FIFA ikiwemo UEFA kuachana nayo
Katika msimu huo Yanga ni miongoni mwa timu tano zilizokusanya alama nyingi katika michuano ya CAF
Al Ahly mabingwa wa CAF CL ndio vinara wakikusanya alama 30, wakifuatiwa na Wydad Casablanca iliyocheza fainali ya ligi ya mabingwa ikikusanya alama 25
Wydad wamefungana na USM Alger waliotwaa taji la CAF CC wakikusanya alama 25 pia
Yanga, Mamelod Sundowns na Esperance zote zimekusanya alama 20 kuwa miongoni mwa timu tano zilizokusanya alama nyingi zaidi katika mashindano ya CAF msimu uliopita
Kwa mujibu wa takwimu za ubora zilizotolewa na CAF kuelekea msimu mpya wa mashindano ya Shirikisho hilo, Yanga imesogea hadi nafasi 18 kutoka nafasi ya 75 waliyokuwa wakishika msimu uliopita
Kama msimu huu Yanga itarudia kile iliyofanya msimu uliopita kwa angalau kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, basi tutarajie kuwaona Wananchi kwenye 10 bora msimu ujao
Droo ya mechi za awali na raundi ya kwanza kwa Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho inafanyika leo huko Misri