Nahodha msaidizi wa kikosi cha Yanga Thabani Kamusoko amesema wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Township Rollers.
Kamusoko ambaye leo aliiwakilisha Yanga kwenye Mkutano na Waandishi wa habari akiwa sambamba na kocha Msaidizi, Noel Mwandila, amesema bencho la ufundi limefanyia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza hivyo wana matumaini ya kuibuka na ushindi mnono kesho.
"Township Rollers ni timu nzuri tunaiheshimu na tumeona mpira wake kikubwa naamini tumejipanga kuibuka na ushindi kwa kuwa mwalimu amefanyia kazi makosa yote ya mchezo uliopita," amesema Kamusoko.
Kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam March 07, Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 na sasa inalazimika kuhinda kwa idadi sawa na hiyo ya mabao huku ikihakikisha hairuhusu bao.

ADVERTISE HERE