Mshambuliaji Yusuf Athumani amejiunga na klabu ya West Armenia barani Ulaya
Yusuf ametua timu hiyo ya Armenia inayoshiriki ligi daraja la kwanza. Ataitumikia kwa mkopo wa msimu mzima
Yanga imethibitisha kumtoa Yusuf kwa mkopo baada ya kumaliza kuitumikia Coastal Union kwa mkopo wa miezi sita
Yusuf alianzia maisha yake ya soka Yanga B kabla ya kusajiliwa na klabu ya Biashara United aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa
Baadae Yanga ikamrejesha kikosini wakimpa mkataba wa miaka mitatu
Hii ni nafasi kwake kwenda kuimarisha kiwango chake na pengine kufungua milango zaidi ya fursa barani Ulaya
Kila la kheri Yusuf...!
ADVERTISE HERE