Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amesema hakuna uwezekano Yanga ikamruhusu kiungo wake Jonas Mkude 'Nungunungu' aondoke kambini akaagwe katika Tamasha la klabu nyingine
Kamwe amesema wale wanaotaka kumuaga wahakikishe wanahudhuria kilele cha Wiki ya Mwananchi uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi Julai 22, watapewa nafasi ya kumuaga lakini sio vinginevyo
"Mkude ni mchezaji wa Yanga sasa, kama wanataka kumuona au kumuaga kwa mara ya mwisho, mahali pekee wanapoweza kuja kumuona ni kwenye kilele ya Wiki ya Mwananchi"
"Kwa hiyo kama wanataka kumuaga tunawakaribisha waje siku ya Jumamosi Julai 22, 2023 tutawapa nafasi ya kusimama na kumpigia hizo salute na parade halafu tutawaruhusu watoke waende kuendelea na shughuli nyingine"
"Mkude yupo kwa ajili ya Yanga na kuwapa furaha wanayanga, ataonekana siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi pekee. Wengine labda wanaweza kuongea na mamlaka za wanyama pori wakamchukua Nungunungu mwingine wakampeleka kwenye tamasha lao lakini Nungunungu kwa maana ya Jonas Mkude kama wanataka kumuaga waje siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi, tunawakaribisha," alitamba Kamwe