Kocha Mkuu wa Yanga SC, George Lwandamina amesema kwamba kambi ya kikosi chake ipo vizuri kuelekea mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Township Rollers keshokutwa mjini Gaborone.
Yanga SC iliyofikia katika hoteli ya Crystal Palace mjini Gaborone inatarajiwa kuteremka Uwanja wa Taifa wa Gaborone JumamosiSaa 10:45 kwa saa za Afrika Mashariki kwa mchezo huo, wakihitaji ushindi wa 2-0 ili kwenda hatua ya makundi baada ya kufungwa 2-1 Dar es Salaam Jumanne ya wiki iliyopita.
Katika mahojiano na mtandao wa Bin Zubeiry, Lwandamina amesema kwamba wanaendelea vizuri na maandalizi na wachezaji wote wapo vizuri
“Tunamshukuru Mungu tunaendelea vizuri na maandalizi yetu, soka ya Afrika inafanana hata maeneo na vifaa vya mazoezi,â€amesema.
Kuhusu wagonjwa au majeruhi katika timu, Lwandamina amesema; “Soka ni mchezo wa nguvu hivyo huwezi kutarajia timu kutokuwa na mchezaji mwenye maumivu kabisa, kwa sababu Yanga imekuwa katika msimu mgumu huuâ€.
Wakati huo huo; Balozi wa Tanzania nchini Botswana, Sylvester Ambokile jana jioni aliitembelea kambi ya Yanga na kula chakula cha jioni na kuzungumza na wachezaji kuwapa moyo kuelekea mechi hiyo.
Wachezaji waliopo na Yanga SC mjini Gaborone ni pamoja na makipa; Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, mabeki Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.
Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Yussuf Mhilu, Pius Buswita, Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Juma Mahadhi, Ibrahim Ajib, Thabani Kamusoko, Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya.
Upande wa viongozi ni pamoja na kocha Mkuu, Lwandamina, wasaidizi wake Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli Jacob Onyango na Meneja Hafidh Saleh wakati viongozi ni Omar Kaaya, Samuel Lukumay na Elias Mwanjala.

ADVERTISE HERE