Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kesho Jumatano anaanza rasmi majukumu ya kuwanoa mabingwa hao wa Tanzania Bara katika pre-season ya 2023/24
Gamondi mwenye uraia pacha wa nchi za Argentina na Italia, tayari ameandaa program ya pre-season ambayo itaanza Avic Town
Huenda leo Yanga ikatangaza benchi la ufundi ambalo litakuwa chini ya Gamond kuhakikisha wanaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika misimu miwili iliyopita
Meneja wa Yanga Walter Harrison jana aliwaambia Wanahabari kuwa wachezaji wamerejea ambapo leo watakamilisha vipimo vya afya tayari kuanza mazoezi
Gamondi ameahidi kutengeneza kikosi imara chenye ushindani ili kuhakikisha Yanga inaendeleza ubabe katika michuano mbalimbali msimu ujao
Kama ilivyokuwa kwa Profesa Nasreddine Nabi, Gamondi ni kocha anayependa soka la kasi linaloambatana na pasi fupi 'tiki-taka'