Klabu ya Yanga imetoa taarifa kuwa winga Denis Nkane anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya dharua Hospitalini
Nkane alipata majeraha baada ya kuangukia kichwa katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets uliopigwa jana huko Malawi kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi
Nkane alipewa huduma ya kwanza uwanjani kabla ya kupelekwa Hospitalini kwa matibabu zaidi, hali yake inaendelea vyema
Kikosi cha Yanga kimerejea nchini Tanzania baada ya mchezo huo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana
ADVERTISE HERE