Wakati Yanga ikipaa kuelekea Malawi mapema leo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliwataka Wananchi kupuuzia taarifa zinazodai wameporwa mchezaji kwa kuwa jambo hilo haliwezi kutokea
Hersi amesema hiki ni kipindi cha usajili hivyo anafahamu zinazungumzwa tetesi nyingi lakini zenye ukweli ni chache
"Itakuwa ajabu sana kwa mchezaji awe anatakiwa sehemu halafu afike airport atoroke, najua huu ndo muda wenu wa kuzungumza mambo mengi si kipindi cha eetesi," alisema Hersi
Hata hivyo ni kama propaganda hiyo iliyoibuliwa ili kupamba usajili wa mchezaji Fabrice Ngoma aliyekuwa akitajwa kutua Simba, imeingia mchanga baada ya jana klabu ya Al Hilal kutangaza kuwachukulia hatua wachezaji wake watatu Lamine Jarjou, Fabrice Ngoma na Ibrahim Imoro kwa kutoroka kambi ya timu hiyo huko Tunisia
Wachezaji hao wanadaiwa kuandika barua za kuvunja mikataba yao pasipo kufuata utaratibu, Al Hilal imewasilisha malalamiko yake FIFA