Ni heshima Yanga kualikwa Malawi - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2023
Ni heshima Yanga kualikwa Malawi - Hersi

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mwaliko waliopata kushiriki sherehe za Uhuru huko Malawi ni ishara ya heshima kubwa ambayo timu hiyo inapewa nje ya nchi

Hersi ameongoza msafara wa Yanga ambao umeondoka mapema leo kuelekea Malawi ambako Alhamisi watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Malawi

"Ni heshima kubwa kwa Klabu ya Yanga kushiriki kwenye matukio makubwa kama haya, wote tunajua sherehe namba moja kwenye nchi ni uhuru"

"Sisi kualikwa ni heshima kubwa kwa Yanga na inaonyesha utayari wa Mataifa mengi kushirikiana na Yanga. Tanzania kuna Klabu nyingi wangeweza kualikwa, ni heshima kubwa sana sisi kualikwa tunawashukuru watu wa Malawi," alisema Hersi

Kikosi cha Yanga kimeondoka nchini leo kwa Ndege maalum ambayo itawarudisha baada ya mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets hapo kesho

Msafara wa Yanga haujawajumuisha baadhi ya wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza wakipewa mapumziko baada ya msimu wa mafanikio 2022/23

Yanga itaingia rasmi kambini Julai 10 kuanza maandalizi ya msimu mpya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’