Msafara wa Yanga unaondoka nchini leo majira ya asubuhi kuelekea Malawi ambako watacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bullets siku ya kesho
Ni mwaliko kutoka Serikali ya Malawi katika maadhimisho ya Uhuru wa nchi hiyo ambayo yatafanyika kesho Julai 06
Yanga inatarajiwa kuondoka na msafara wa takribani wachezaji 21 ambao utajumuisha wachezaji 15 wa kikosi cha kwanza na wachezaji sita wa timu ya vijana
Nyota mpya aliyesajiliwa katika dirisha hili la usajili Nickson Kibabage ni miongoni mwa wachezaji watakaosafiri
ADVERTISE HERE