Hatma ya Mkude mikononi mwa Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2023
Hatma ya Mkude mikononi mwa Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Angel Gamondi ndiye atakayeamua hatma ya kiungo Jonas Mkude kusajiliwa Yanga au la

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema hakuna timu haitapenda kuwa na mchezaji kama Mkude ambaye ana uzoefu mkubwa wa soka la Tanzania na hata Kimataifa

Kamwe amesema kama Gamondi atapendezwa na kiungo huyo basi Wanachama na Mashabiki wa Yanga watarajie kumuona katika kikosi chao msimu ujao

"Mkude ni miongoni mwa viungo bora wa kuzuia nchini, ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na soka la Tanzania"

"Ikitokea kocha (Gamondi) amemuhitaji basi atasajiliwa kwani tunaamini atakuwa na mchango mkubwa katika klabu yetu. Sio Yanga tu, hata kama atasajiliwa na timu nyingine tutaamini mchango wake utakuwa mkubwa," alisema Kamwe

Mkude ameibua mjadala baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa Yanga imempa mkataba wa mwaka mmoja

Baada ya kuhusishwa na Yanga, waliokuwa waajiri wake Simba wameibuka na kudai wanatambua thamani ya mchezaji huyo na watafanya tukio kubwa la kumuaga katika Tamasha la Simba Day

Miongoni mwa waliohoji kauli ya Simba iliyotolewa baada ya Mkude kuhusishwa na Yanga ni Kamwe ambaye alisema hana uhakika kama timu yake mpya itamruhusu aache pre-season ili aende akaagwe

"Yani mchezaji yuko pre-season na timu yake mpya halafu mnamwambia aje ili aagwe, mlikuwa wapi kufanya jambo hilo mapema? Kwani hamkujua kama hamtaendelea nae?"

"Sisi tulimuaga Haruna Niyonzima kwenye mechi ya mwisho ya msimu wa ligi kuu. Hivi ndivyo timu kubwa hufanya. Nasubiri kuona kama hiyo timu yake mpya itamruhusu aache pre-sesaon ili mumuage, nimekaa pale.....!" 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’