Nimesikia jana baada ya Yanga kupitia Mkutano Mkuu kutangaza bajeti kwa msimu ujao kuwa Bil 20.8, watani zao nao wakajibu mapigo katika hafla iliyoandaliwa na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa Simba
Kupitia hafla hiyo, Mtendaji wa Simba akatangaza kuwa bajeti yao ni Tsh Bilioni 23 lengo likiwa kuwaonyesha mashabiki kuwa wao ni wakubwa zaidi ndio maana hata bajeti yao ni kubwa!
Hata hivyo Januari 29 wenye kumbukumbu wanafahamu Simba walitangaza bajeti yao ya msimu ujao kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama kuwa ni Tsh Bilioni 13.7. Kwa waliosahau ni katika ule Mkutano ambao mchezaji Cesar Manzoki alialikwa!
Kwa sasa ni wazi Yanga imepiga hatua kubwa kuliko watani zao Simba, ndio maana kila wanachokifanya lazima upande wa pili wasake majibu hata ya kisiasa
Yanga iliposaini mkataba wa udhamini wa SportPesa wenye thamani ya takribani Tsh Bilioni 4 kwa mwaka, Simba nao wakatangaza kuingia mkataba wa M-Bet uliodaiwa kuwa na Thamani ya zaidi Tsh Bilioni 5 kwa mwaka (Bil 26 miaka mitano)
Yanga ilipotinga fainali ya Shirikisho barani Afrikam nguvu kubwa ikatumika kuuambia UMMA kuwa hata Simba nao walicheza fainali ya CAF mwaka 1993 pamoja na kuwa CAF wenyewe katika taarifa zao wamebainisha kuwa Yanga ndio klabu ya kwanza kutoka Tanzania kucheza fainali ya mashindano ya CAF
Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said, imejipambanua na kujikita zaidi katika kutimiza mipango na mikakati yao wanayojiwekea na sio kushindana na wengine
Katika vikao vya Yanga, kinachozungumzwa zaidi ni ajenda lakini huko kwa watani zao sehemu kubwa ya mijadala ni kutaka kujionyesha ni wakubwa