Zinavuna kila kona tetesi kuhusu kiungo Jonas Mkude ambaye hataendea kuitumikia klabu ya Simba baada ya mkataba wake kumalizika
Zipo taarifa za ndani kuwa mabosi wa Yanga wanaweza kumpa Mkude mkataba wa mwaka mmoja wakiamini anaweza kuongeza kitu katika kikosi cha Yanga
Mkude ni miongoni mwa viungo bora walioyajenga majina yao katika soka la Tanzania kwa muda mrefu
Yawezekana kwa sasa sio yule Mkude wa misimu kadhaa iliyopita lakini bado ni mchezaji anayeweza kuongeza kitu kwenye timu
Hata hivyo huku Yanga eneo la kiungo tayari lina Yannick Bangala, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Salum Abubakar na Zawadi Mauya huku Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe akitamba kuna namba 6 mwingine matata atatambulishwa wiki ijayo
Je atasajiliwa?Β Tusubiri...!
ADVERTISE HERE