Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Angel Gamondi ameshiriki kikamilifu maboresho ya kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao wa mashindano
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa Yanga ilianza Mawasiliano na Gamondi kabla ya msimu kumalizika baada ya Kocha Nasreddine Nabi kuwataarifu hataendelea kuinoa Yanga
"Maboresho ya kikosi chetu yamezingatia mapendekezo ya Mwalimu Gamondi. Tumekuwa na mawasiliano nae na kumshirikisha katika kila hatua"
"Niwaibie siri hata huyo namba sita ambaye tutamtambulisha, usajili wake umeidhinishwa na Gamondi"
"Wachezaji wa kigeni tuliowasajili na hata wa ndani amewafuatilia kupitia mechi walizocheza. Mwalimu amepata muda wa kutosha kuwafuatilia wachezaji na kutoa mapendekezo yake pale ilipohitajika," alisema Kamwe
Kamwe amesema baada ya utambulisho wa jezi ambao utafanyika wiki ijayo, wataanza kutambulisha wachezaji waliowasajili