Yanga U20 ni kama imeondolewa katika ligi kuu ya vijana mapema baada ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Dodoma Jiji na Tanzania Prisons
Vijana wameshindwa kuilinda heshima iliyowekwa na kaka zao katika soka la Tanzania kwa misimu miwili mfululizo
Katika mechi mbili, Yanga U20 wameruhusu mabao manne huku wenyewe wakipachika bao moja tu
Walifungwa 1-0 na Dodoma Jiji kabla ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tanzania Prisons hapo jana
Said Maulid 'SMG' ndiye mkufunzi wa Yanga U20, amekiri msimu huu hawajawa na timu yenye ushindani
Pengine uongozi wa Yanga unapaswa kuweka sawa utaratibu wa upatikanaji wa wachezaji wanaosajiliwa na timu hiyo
Ikiwezekana, timu itafutiwe udhamini ili kupanua wigo wa kutafuta vipaji hata nje ya jiji la Dar es salaam