Ni fahari kujiunga na timu kubwa Afrika - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2023
Ni fahari kujiunga na timu kubwa Afrika - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Angel Gamondi amesema ana furaha kujiunga na moja ya timu kongwe na kubwa barani Afrika na yenye mashabiki wengi

Gamondi amesema ni matumaini yake kwa ushirikiano na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki, mafanikio yataendelea Jangwani

Gamondi raia wa Argentina alitangazwa jana kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi ambaye anatajwa kuwa mbioni kujiunga na Kaizer Chiefs

"Nimekuwa nikifundisha kwa zaidi ya miaka 20 barani Afrika. Nilifundisha vilabu vikubwa kama CR Belouizdad, Sundowns, ES Tunis na Wydad. Nilikuwa na bahati ya kupata matokeo mazuri na mafanikio pamoja nao"

"Nafurahi kujiunga na Yanga. Kwangu mimi, ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi na historia. Ni moja ya klabu kubwa barani Afrika"

"Ninaamini, ikiwa tunaweza kufanya kazi pamoja; mashabiki, menejimenti, wachezaji na wafanyakazi wa kiufundi tunaweza kuendelea kuleta mafanikio na mafanikio makubwa zaidi," alisema

Gamondi anakuwa Kocha wa pili kutoka Amerika Kusini kuinoa klabu ya Yanga baada ya Marcio Maximo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’