Bajeti ya Yanga msimu wa 2023/24 ni Tsh Bilioni 20.8, hii ni ishara ya malengo makubwa yaliyowekwa kwa msimu ujao
Huu ndio wakati ambao maji na mafuta vinajitenga! Kwani wakati wengine wakitamba ni wakubwa, thamani ya uwekezaji wao ni sawa na bajeti ambayo Yanga wameiweka kwa msimu mmoja!
Kwa lugha nyingine Yanga wanaweza kuwasilisha maombi ya kuinunua timu mojawapo hapo Kariakoo, wakaibeba na salio likabaki!
Aidha ujio wa Kocha Miguel Gamondi ni ishara nyingine ya malengo makubwa ya Yanga
Kocha aliyefundisha timu zenye mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika. Gamondi anafahamu nini kifanyike ili timu iweze kupata mafanikio kwenye soka la Afrika
Msimu uliopita Yanga imecheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, msimu ujao Wananchi wanataka mafanikio makubwa zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Huu moto wa makombe Yanga sio wa kuzimika leo au kesho...!