Tukio kubwa litakalojiri kesho Jumamosi, Juni 24 ni Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere ukiwa Mkutano wa mwaka
Shauku imekuwa kubwa kwa Wanachama na Mashabiki wa Yanga kufahamu mikakati ya timu yao kuelekea msimu ujao
Kupitia Mkutano huo Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ataweka wazi mikakati hiyo pamoja na masuala muhimu yanayoihusu Yanga
Lakini muhimu zaidi, kwenye Mkutano huo huenda Wananchi wakapata habari njema kuhusu masuala ya usajili
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya ukimya, muda wa kuwapa furaha Wananchi umefika
Kwa kuanzia Kamwe amesema tayari Injinia Hersi amekamilisha usajili wa kiungo matata ambaye atakabidhiwa jezi namba sita iliyokuwa ikitumiwa na Feisal Salum 'Fei Toto'
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kamwe ameanzisha shindano maalum akiwataka Wananchi kutumia ubunifu kuchora namba sita akiahidi kutoa zawadi
Huo ni mwanzo wa maandalizi ya kumpokea kiungo huyo matata ambaye Injinia Hersi amefanikiwa kumshusha Jangwani
Lakini pia Yanga haijatangaza kocha mkuu, taarifa imetolewa Kocha atatangazwa baada ya Mkutano Mkuu